Ander Herrera aliekua kiungo wa Paris saint German ya nchini Ufaransa amerejea klabu yake ya zamani ya Athletico Bilbao ya nchini Hispania.

Nyota huyo alieitumikia PSG kwa misimu kadhaa na kufanikiwa kushinda mataji kadhaa likiwemo taji la ligi kuu maarufu kama Ligue 1,Cope de france,pamoja na French super cup  akitokea klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza amejiunga na klabu yake hiyo ya zamani ya Bilbao kwa mkopo wa msimu mzima kukiwa na kipengele cha kumnunua jumla kiungo huyo wa kihispaniola.

ander herrera, Ander Herrera Arejea Nchini Hispania, Meridianbet

Kiungo huyo anaamua kutafuta changamoto kwenye timu nyingine kwajili ya kupata nafasi zaidi ya kucheza baada ya kuonekana kuna ufinyu wa nafasi kwenye kikosi cha mwalimu Galtier.

Sajili mpya zilizoingia kwenye kikosi cha PSG wakati huu wa majira ya joto kwenye eneo la kiungo kumemuweka Herrera kwenye wakati mgumu klabu hiyo imeongeza wachezaji kama Vitinha, pamoja na Renato Sanches wachezaji hawa ndo cha ya kiungo huyo wa kihispaniola na kutafuta changamoto nyingine.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa