Golikipa wa Manchester United Andre Onana amesema anaamini atarejea kwenye ubora wake ambao amekua nao. Golikipa huyo amezungumza hivo kutokana na maneno mengi yanayotupwa kwake kwa kuonekana kashuka kiwango.
Andre Onana ameeleza kua haiwezekani golikipa bora kwenye michuano ya ulaya kwa miezi sita nyuma awe kipa mbaya duniani sio kweli, Lakini akiamini kua kila kitu kitakua sawa ndani ya Manchester United.Golikipa huyo amekua kwenye kiwango cha chini tangu amejiunga na Manchester United kwenye dirisha kubwa lililopita, Lakini anaamini kila kitu kitakua sawa ndani ya klabu hiyo na ni suala muda tu yeye kurejesha ubora wake.
Golikipa huyo raia wa kimataifa wa Cameron amekua hana msimu mzuri ndani ya kikosi cha Mashetani wekundu mpkaka sasa, Huku akiwa amefanya makosa kadhaa ambayo yameigharimu timu hiyo katika michezo tofauti tofauti.Matumaini ni makubwa kwa Andre Onana licha mwanzo mgumu alioanza nao klabuni hapo yeye anaamini atakaa sawa na aterejesha kiwango chake ambacho alikua anakionesha kwenye vilabu vyake kadhaa ambavyo amepita kama Inter Milan na Ajax ya nchini Uholanzi.