Golikipa wa Ajax, Andre Onana amefunguka kuwa anatamani kuondoka klabuni hapo. Onana amekuwa akihusishwa na klabu ya Barcelona wakati akiwa anasisitiza kuwa anataka kupiga hatua zaidi.

Onana, mwenye miaka 24, ameichezea klabu klabu hiyo tangia alipofika kutoka Barcelona mwaka 2015.

Golikipa huyu amekuwa akizivutia klabu kadhaa kubwa Ulaya ambazo tayari zimeonesha nia ya kumtaka kuboresha vikosi vyao, wakiwemo Barcelona, Chelsea na Tottenha.

Andre Onana Anatamani Kusepa Ajax, Apige Hatua Zaidi
Andre Onana

Onana ansema kuwa alikuwa tayari kuondoka klabuni hapo, lakini alikluwa anatarajia kupiga hatua zaidi kama angeondoka. Alitamani apate klabu kubwa zaidi, kama hatua moja kubwa ya mafanikio katika soka lake la kulipwa.

Staa huyu bado ana mkataba na Ajax ambao utadumu hadi mwaka 2022 ikiwa hakutatokea mabadiliko hapa karibuni.

Katika mahojiano na AD jumanne, alibainisha kuwa licha ya ukweli kuwa alitamani kuondoka klabuni hapo, asingependa kueleweka vibaya, ni katika jitihada za kupiga hatua zaidi.

“Msinifikirie vibaya, nina furaha sana hapa Ajax na ninaishukuru sana klabu. Imekuwa miaka mizuri mitano hapa, lakini sasa wakati wangu umefika wa kupiga hatua. Tulifanya hayo makubaliano mwaka uliopita. Sijui nini kitatokea lakini ninachohitaji na makubaliano yetu yako wazi” -Andre Onana

4 MAONI

  1. Tena ikiwezekana kikomochake kikifikia 2022 wakubaliane nae kama kuna club anayoitaka ikifikia makubaliano au ikimuitaji akacheze aende wasimpe longolongo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa