Andre Onana na Maguire Waibuka Mashujaa

Golikipa wa klabu ya Manchester United Andre Onana na beki Harry Maguire wamefanikiwa kuibuka mashujaa katika mchezo wa jana wa ligi ya mabingwa ulaya katika mchezo wao dhidi ya FC Copenhagen.

Andre Onana alikua shujaa wa dakika za usiku kabisa baada kuokoa mchomo wa penati baada ya kuongoza goli moja kwa bila, Lakini golikipa huyo alikua kwenye ubora wake katika mchezo wa jana.ANDRE ONANABeki Harry Maguire ndio aliowapa uongozi Manchester United dakika ya 72 ya mchezo na kushikilia uongozi huo mpaka dakika ya 90 ya mchezo, Mpaka pale ambapo ilipatikana penati na kuchomolewa na golikipa Onana.

Beki Harry Maguire amekua akitupiwa lawama kwa takribani mwaka sasa kutokana na kua chini ya kiwango, Lakini hivi karibuni amekua akionesha ubora katika mechi alizopewa nafasi ikiwemo mchezo wa jana ambapo alifunga bao la ushindi.ANDRE ONANABaada ya matokeo ya ushindi katika mchezo wa jana ambayo Manchester United ilipata matokeo ya ushindi na wachezaji Andre Onana, Harry Maguire kuonesha ubora mkubwa inaweza kua sehemu ya kurejesha hali ya kujiamini katika michezo ijayo.

Acha ujumbe