Taarifa zinasema beki wa Chelsea, Andreas Christensen tayari amekubali kuungana na Barcelona.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano na Mundo Deportivo, nyota huyu tayari amekubali kuungana na Barcelona kwa dili la miaka 5.
Mkataba wa Andreas Christense na Chelsea unamalizika Juni 30, na kwa takribani wiki kadhaa Barcelona wamekuwa wakizungumza na wakala wa staa huyu.
Ikiwa dili hili liko sawa, basi Andreas Christensen anatarajia kuwasili Camp Nou, Mateu Alemany na Jordi Cruyff watasafiri kukamilisha jambo hilo huko London.
Christensen ana umri wa miaka 25 tu, lakini tayari ana uzoefuy mkubwa na ni sehemu muhimu ya kikosi cha Chelsea kilichowachapa Man City kutwaa Ubingwa wa UCL kule Porto.
Bayern Munich pia walitajwa kuiwania saini yake, lakini staa huyu anatajwa kuwa na mahaba ya kuichezea Barcelona chini ya Xavi Hernandez.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.