Andreas Christensen amevumilia majuma machache magumu akiwa na klabu yake.

Beki huyo wa kati wa Chelsea atajiunga na Barcelona kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu huu lakini amekuwa akicheza chini ya kiwango katika klabu hiyo ya London kwa wiki kadhaa sasa kwa mujibu wa Diario Sport.

Andreas Christensen
Andreas Christensen

Beki huyo wa Denmark alikaliwa kooni wakati wa mapumziko Chelsea ilipochapwa na Arsenal kwenye Uwanja wa Stamford Bridge Jumatano jioni, kama vile alivyokuwa dhidi ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa.

Cesar Azpilicueta, ambaye pia anatarajiwa kuelekea Camp Nou msimu huu wa joto, alikuwa kando yake kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea lakini hakuwa na uwezo wa kuzuia kipigo cha bao 4-2 dhidi ya Arsenal.

Barcelona wanasemekana kuingiwa na wasiwasi kutokana na kushuka kwa ghafla kwa kiwango cha Andreas Christensen, hasa kutokana na rekodi yake ya majeruha. Lakini imani inabaki kuwa atakuwa na ubora huko Barca.

Christensen, 26, alijiunga na Chelsea mwaka 2012 akitokea Brondby. Ametumia maisha yake yote ya ujana Stamford Bridge ukiacha miaka miwili ya mkopo kule Bundesliga akiwa na Borussia Monchengladbach.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa