Ange Amsifu Richarlison Huku Spurs Ikipata Ushindi Mnono

 

Ange Postecoglou amefurahishwa na Richarlison kufuatia matokeo yake katika ushindi wa 2-1 wa Tottenham dhidi ya Sheffield United dakika za lala salama.

 

The Blades walionekana kuimarika katika njia yao ya kupata ushindi wao wa kwanza katika kampeni za Ligi Kuu ya 2023-24 baada ya Gustavo Hamer kuwafunga vijana wa Paul Heckingbottom kwa bao 1-0 katika dakika ya 73.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa Brazil aliingia akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha la Spurs dakika nane kabla ya 16 iliyoongezwa kabla ya kumtengenezea Dejan Kulusevski bao la ushindi.

Baada ya ushindi huo, Postecoglou alisifu uchezaji wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na kuamsha maisha ya Spurs.

Alisema: “Tunapaswa kudumisha usawa katika maisha na hata kwake Richarlison, anahitaji kuelewa soka lake bado ni zuri, ni mwanasoka mzuri. Ana mengi ya kutoa na hiyo inaweza kusaidia kupunguza mzigo anaohisi katika sehemu zingine za maisha yake, kama wengi wetu.”

Ange amesema kuwa amefurahishwa sana naye akisema alifikiri alifanya vizuri sana. Ni wazi walikuwa wakifuata bao na kupata mipira kwenye eneo la hatari na huwa tishio angani.

Pia alipongeza moyo wa wachezaji wake kurejea mchezoni kuna ujasiri na roho ndani ya kundi hilo tayari ambayo ni nzuri kuona kwa sababu ni kundi jipya.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Wakati huo huo, kocha wa Blades Heckingbottom alikasirishwa na mwamuzi wa mechi hiyo.

Alisema: Kuna kitu kinahitaji kufanywa sasa. Na huyu sio mimi ninayelalamika, nilisema wakati wa mapumziko na tulipokuwa mbele kwa bao 1-0 pia.

“Kipaumbele ni kupoteza muda kwa hiyo waamuzi wanatuelekeza jinsi tunavyocheza, tunapanga kutoka nyuma, kisha Spurs wanasonga mbele na hapo ndiyo inaelekeza jinsi tunavyocheza. Lakini hapana, tunaambiwa tucheze kwa muda mrefu, huwezi fanya.”

Wes Foderingham alipata kadi ya njano kwa kucheza nje ya eneo la hatari na kutishiwa kupewa kadi nyekundu kwa kupoteza muda huwezi kufanya hivyo.

“Wasiwasi wangu ni kwamba umakini wangu uko kwenye kadi za njano kwa kupoteza muda na nilipozungumza na waamuzi hawakuelewa ninachozungumzia. Wao ndio wasimamizi wa mchezo, hawajui mchezo. ” Alisema kocha huyo.

Acha ujumbe