Ange Postecoglou Malengo Makubwa Spurs

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Ange Postecoglou ameweka wazi malengo yake ndani ya klabu yake kuelekea msimu ujao ambapo ana mipango mikubwa zaidi ya msimu huu.

Ange Postecoglou amesema hatarajii kuridhika na nafasi ambayo watamaliza msimu huu kwasababu yupo ndani ya Spurs kwasababu ya kushinda na anataka kushinda, Hii inaonesha kwa kiasi gani kocha huyo ana njaa ya mafanikio ndani ya timu hiyo.ange postecoglouKocha huyo amesema nafasi watakayomaliza nayo msimu huu itakua msingi mzuri wa kuelekea msimu ujao, Hivo kama msimu huu watamaliza kwenye nafasi nzuri hiyo itakua na maana msimu ujao watahitaji kufanya zaidi wa waliyoyafanya msimu huu.

Tottenham mpaka sasa wanashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku malengo yao yakiwa kumaliza katika nafasi nne za juu ili waweze kurejea katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.ange postecoglouKocha Ange Postecoglou mipango yake mikubwa zaidi msimu huu ni kuhakikisha anaiweka klabu hiyo ndani ya nafasi nne za juu, Huku mipango ya kuwania ubingwa itakua msimu ujao ambapo atahitaji kuendeleza alipoishia msimu huu kwani yupo kwneye timu hiyo kwasababu anataka kushinda.

Acha ujumbe