Antony ameweka wazi kuwa bado anaendelea kuifuatilia Manchester United baada ya kutazama ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Liverpool Jumatatu usiku.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa mmoja wa walengwa wakuu wa United kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi lakini Ajax wamesimama kidete juu ya dau lao la Euro milioni 100 (£84.8m).

Wiki iliyopita, Antony alikataa kufanya mazoezi na klabu hiyo ya Uholanzi na kukemea ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Sparta Rotterdam siku ya Jumapili alipokuwa akijaribu kulazimisha kuhamia Man United.

manchester united, Anthony bado anaitaka Manchester United., Meridianbet

Inaonekana Antony anafuatilia kwa karibu maendeleo ya Man United chini ya kocha Erik ten Hag alipotuma picha pamoja na kaka yake kwenye mtandao wa kijamii wakati akitazama mchezo dhidi ya Liverpool.

manchester united, Anthony bado anaitaka Manchester United., Meridianbet

Emerson Santos, ambaye pia ni meneja wa Antony, alijumuisha emoji kuashiria anawakubali mashetani wekundu alipokuwa akipiga picha ya moja kwa moja ya mchezo wa United kwenye televisheni yake.

manchester united, Anthony bado anaitaka Manchester United., Meridianbet

Inafahamika kuwa Antony ana nia ya kujiunga na United kabla ya dirisha kuisha, huku mtandao wa De Telegraph ukiripoti kuwa Ajax haijafurahishwa na uamuzi wa Ten Hag kushinikiza kumsajili nyota wao.

Akizungumza wikendi, kocha mkuu wa Ajax Alfred Schreuder alisema anatarajia Antony kusalia Ajax.

“Nataka tu Antony abaki, kwa hivyo nadhani hatauzwa, pesa inayozungumziwa ni ndogo mno, lakini tayari tumeshauza wachezaji watano au sita. Sidhani kama ni sawa iwapo tutauza mchezaji mwingine” Schreuder aliiambia ESPN.

Alipoulizwa kama Ajax wako katika nafasi ya kukataa ofa kubwa kutoka kwa United, Schreuder alisema:

“Siwezi kuhukumu hilo, klabu inapaswa kuhukumu hilo, lakini nadhani tuna nguvu sana kifedha”

Alipoulizwa kama anaamini Antony atasalia Ajax msimu huu wa joto, Schreuder alijibu:

“Hisia zangu kuhusu hilo ni nzuri, lakini pia ninamuelewa kijana huyo, ni vigumu kukubali, Lakini tunacheza Ligi ya Mabingwa na sidhani kama Manchester United inafanya hivyo. Tutaona kitakachotokea”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa