Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Anthony Martial na timu ya taifa ya Ufaransa amewasili leo kwenye kiwanja cha mazoezi cha klabu hiyo maarufu kama Carrington.anthony martialMshambuliaji huyo ambaye amekua akisumbuliwa na majeruhi mara kwa mara ndani ya kikosi hicho licha ya kuonekana kua tegemeo kwenye kikosi cha mwalimu mpya kwenye timu hiyo Eric Ten Haag.

Anthony Martial ambae amjeraha ya mwisho aliyapata wiki mbili zilizopita katika mchezo dhidi ya Everton ambapo nafasi yake kwenye mchezo huo ilichukuliwa na Cristiano Ronaldo ambae alifunga bao la ushindi katika mchezo huo.anthony martialKuonekana kwa Anthony Martial leo kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo kumeleta matumaini kwa mashabiki wa klabu ambao wanamuona mchezaji huyo kama mtu pekee ambao anaweza kuwasaidia kufunga mabao kwenye timu kwani washambuliaji waliopo kama Marcus Rashford ambae anaonekana kukosa magoli mara kwa mara.

Kama mshambuliaji huyo amerejea kikosini itampa nafasi kocha wa timu hiyo kua na machaguzi mengi kwenye eneo la ushambuliaji la klabu hiyo huku pia ikiboresha safu ya ushambuliaji wa timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa