Anthony Taylor Ashushwa Daraja

Mwamuzi Anthony Taylor amekumbana na rungu la shirikisho la soka nchini humo na kushushwa daraja baada ya kuizawadia klabu ya Newcastle mkwaju wa penati katika mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita.

Mwamuzi Anthony Taylor imebainika kua mkwaju aliowazadia Newcastle katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Wolves ambao ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili ulikua wa makosa.anthony taylorMwamuzi huyo kwasasa ataenda kuchezesha ligi daraja la kwanza nchini Uingereza ikifahamika kama Championship badala ya ligi kuu ya Uingereza kutokana na makosa ambayo ameyafanya katika mchezo kati ya Newcastle dhidi ya Wolves.

Mwamuzi huyo mkongwe katika ligi kuu ya Uingereza sio mara yake ya kwanza kufanya maamuzi yenye utata katika michezo mbalimbali ndani ya ligi hiyo, Kwani mwaka jana mashabiki wa klabu ya Chelsea walifanya jaribio la kupiga kura refa huyo kutochezesha michezo yao.anthony taylorMashabiki mbalimbali wameonekana kuipokea kwa shangwe taarifa ya Anthony Taylor kushushwa Championship, Hiyo ikitokana na namna mwamuzi huyo amekua na muendelezo wa makosa katika michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.