Kocha wa klabu ya Tottenham Antonio Conte amepinga vikali kuhusu taarifa ambazo zilikuwa zinazagaa za kumuhusisha kutaka kuhamia kwenye timu inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa  Paris Saint-Germain na kuita uvumi huo ni habari za uongo.

Antonio Conte ambaye amejiunga na klabu hiyo mwezi November mwaka jana lakini tayari ameshahusishwa na kutuka kutimka kwenye klabu hiyo yenye makazi yake London kaskazini, huku taarifa kutoka vyombo vya habari vya Ufaransa vinadai kuwa kocha huyo anataka kazi ya kuinoa klabu ya PSG.

Antonio Conte
Antonio Conte

Kwenye kikao chake na waandishi wa habari leo kabla ya mchezo wake wa siku ya jumapili dhidi ya Leicester city alinukuliwa akisema, “bila shaka, nadhani ni jambo zuri kwa klabu nyingine kuipenda kazi yangu, hili ni jambo moja.

‘Lakini ukweli ni kwamba sipendi watu wanapojaribu kubuni habari, kwa kuzungumza tu, kutengeneza tatizo. Hii sio sawa, na sio haki kwangu, kwa klabu na kwa wachezaji wangu.

‘Pia kwa sababu akili zetu kwa sasa zipo kwenye hii michezo mitano kupata matokeo mazuri kwetu. Narudia tena, ni aina ya jambo linalonifanya ni tabasamu. Lakini nadhani kwamba pia watu wanatakiwa kusema kitu kuhusu hili na kuonesha heshima kwa watu wote waliohusika kwenye hili, na wabuni habari za uongo na kusema maneno yao ya uongo.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa