Antonio Conte amejibu tetesi zinazomhusisha kwenda klabu ya Juventus ya nchini Italia kocha huyo ameonesha kua mkali kutokana na maneno hayo yanayoendelea kuzungumzwa na wandishi mbalimbali.

antonio conte“Ni kunikosea heshima mimi na kocha aliupo katika klabu ya Juventus kwasasa nina furaha hapa kwasasa” Alisema Antonio Conte.

Kocha huyo amezungumza leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa dabi ya London Kaskazini  dhidi ya Arsenal utakaofanyika siku ya jumamosi katika dimba la Emirates.

Kocha huyo amekua akihusishwa  kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani ambayo ameitumikia kama mchezaji na kama kocha kwa mafanikio makubwa lakini amekanusha kutaka kurejea klabuni hapo kama ambavyo vyanzo mbalimbali vinadai huku yeye akisisitiza ana furaha ndani ya spurs hivo hafikirii kuondoka klabuni hapo.

Juventus imeanza msimu vibaya sana kwenye ligi ya nyumbani pamoja na michuano ya Ulaya hivo kupelekea watu wengi kufikiria kocha wasasa klabuni hapo Massimiliano Allegri anaweza kufukuzwa kazi na nafasi yake inahusishwa na Antonio Conte kocha wa zamani wa klabu hiyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa