Meneja wa Tottenham Hotspur Antonio Conte ameripotiwa kupatikana na COVID-19 baada ya kupimwa mwishoni mwa juma.

Muitaliano huyo alikuwa mstari kuhakikisha timu yake iunapata ushindi wa 4-0 dhidi ya Aston Villa Jumamosi iliyopita, huku Son Heung-min akifunga hat-trick akishirikiana na Dejan Kulusevski.

Matokeo hayo yaliifanya Spurs kujisimika katika nafasi nne bora kwenye msimamo wa Ligi ya Premia, Wakiwa pointi tatu juu ya wapinzani wao wa London Kaskazini Arsenal.

Tottenham wanafuatia kucheza dhidi ya The Gunners, lakini taarifa zinaripoti kwamba Conte aliambukizwa virusi vya corona wikendi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Tom Roddy anaongeza, Tottenham bado wanamtarajia Conte kuchukua usukani wa pambano la Jumamosi dhidi ya Seagulls na wana matumaini kwamba hataonesha dalili zozote wikendi.

Mechi dhidi ya vijana wa Graham Potter itakuwa mechi ya 30 kwa Conte akiinoa Tottenham, huku kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Inter Milan akishinda mechi 17 kati ya 29 kwenye usukani hadi sasa.


 

VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa