Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte ameamua kubaki kwenye timu hiyo baada ya kufanikiwa kuingoza kufuzu michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

Antonio Conte baada ya kufanya mazungumzo na mkurugezi Fabio Paratici jijini Turin siku ya ijumaa, ambapo wawili hao inaaminika walizungumza kuhusu usajiri wa majira ya kiangazi, Conte sasa ameamua kubakia Tottenham, kulingana na mteandao wa Telegraph.

Antonio Conte

Tokea Antonio Conte achukue kijiti cha kuinoa klabu hiyo kutoka kwa Nuno Espirito Santo, Conte ameshinda michezo 17 kati ya michezo 28, ambayo ameiongoza klabu hiyo na kufanikiwa kumaliza ligi kwenye nafasi nne za juu.

Antonio Conte Kubaki kwke kwenye klabu hiyo ya kaskazini mwa London, kumeleta neema, baada ya wanahisa wakubwa wa klabu hiyo ENIC, kuamua kuwekeza kiasi cha £150million kama ilivyotangazwa siku ya jumanne, na waliahidi kuwekeza zaidi iwapo kocha huyo atabaki kwenye klabu hiyo.

Uwekezaji huo, utampa nguvu Antonio Conte kuweza kufanya matumizi makubwa kwenye soko la usajiri, ili kushindana na vilabu vingine vikubwa barani ulaya. Pia kubaki kwake kunapelekea mshambuliaji wake Harry Kane, ambaye alikuwa anahusishwa na klabu ya Man City, nae ameamua kubaki kwenye klabu hiyo na hivi karibuni atasaini mkataba mpya.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa