Beki wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger anaripotiwa kuwa atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake ndani ya wiki mbili zijazo.

Staa huyu anamaliza mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa mwezi Juni. Chelsea kwa sasa hawawezi kuongeza mkataba wake kusalia Stamford Bridge kutokana na vikwazo vilivyowekwa kwa mmiliki Roman Abramovich.

Baada ya kujidhihirisha kuwa mmoja wa mabeki wa kati bora katika soka la Ulaya, vilabu kadhaa vikiwemo Manchester United, Juventus, Paris Saint-Germain, Tottenham Hotspur, Real Madrid na Barcelona vimehusishwa na kuhitaji huduma yake.

Kwa mujibu wa The Athletic, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake kabla ya mwisho wa mwezi.

Rudiger anadaiwa kukusanya pauni 90,000 kwa wiki, na amekuwa muhimu mkubwa kwa kikosi cha Thomas Tuchel wakati wa kampeni za 2021-22.

Antonio Rudiger amecheza mechi 47 katika mashindano yote, akichangia mabao matano na asisti nne.

Licha ya kutakiwa na Man United, mabingwa hao mara 20 wa Uingereza wanadaiwa kutokuwa na uhakika wa kumsajili Antonio Rudiger msimu huu wa joto, huku kuhamia nje ya nchi kunaonekana kuwa chaguo kubwa zaidi iwapo ataondoka Chelsea.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa