Aliyewahi kuwa mchezaji na nahodha wa Man United, Antonio Valencia, ameamua kutundika daluga na kuachana na mchezo wa soka kama mchezaji.

Valencia alisajiliwa na United akitokea Wigan Athletic (2009). Alifanikiwa kubeba mataji mawili ya EPL, Kombe 1 la FA Cup, makombe mawili ya Kombe la Ligi, Ngao 3 za hisani na kombe 1 la Europa wakati alipokuwa United.

Licha ya kubeba makombe, Antonio Valencia alitwaa tuzo mbalimbali ikiwemo ya Mchezaji bora wa msimu, goli bora la msimu na mchezaji bora wa msimu aliyechaguliwa na wachezaji wenzake katika msimu wa 2011/12 na 2016/17.

Antonio Valencia, Antonio Valencia Atundika Daluga., Meridianbet
Valencia akiwa na kombe la Europa, 2017.

Safari ya unahodha wa United ilianza kwenye mchezo wa fainali ya Europa dhidi ya Ajax 2017. Baada ya mchezo ule, Valencia alikabidhiwa rasmi kitambaa cha unahodha wa Man United baada ya Wayne Rooney kuondoka Old Trafford.

Tarehe 12 May, 2019. Valencia aliondoka United akiwa ameitumikia klabu hiyo kwa michezo 339 na kupachika magoli 29. Alirejea nyumbani kwao (Equador) kukipiga katika klabu ya LDU Quito kabla ya kujiunga na klabu ya Queretaro ya nchini Mexico ambapo amestaafia huko.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Antonio Valencia, Antonio Valencia Atundika Daluga., Meridianbet

CHEZA HAPA

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa