Antony Awajibu wanaomkosoa

Mchezaji wa Manchester United raia wa Brazil Antony Santos amewajibu watu wanaomkosoa kutokana na aina yake ya uchezaji.

Winga huyo alievunja rekodi ya usajili katika ligi kuu nchini Uholanzi, Kwa kusajiliwa kwa paundi milioni 100 amekua akikosolewa kutokana na aina yake ya uchezaji ambayo imeonekana sio ya kunufaisha timu bali imekaa kimaonesho zaidi.antonyAntony ametumia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwajibu ambao wamekua wakimkosoa kutokana na aina yake ya kuchezea mpira kwa kusema “Tumejulikana kwa sanaa yetu, Na siwezi kuacha kitu kilichonifanya kuwepo hapa nilipo”

Antony ameonekana kukerwa na wakosoaji wanaomkosoa kutokana na uchezaji wake wakiongozwa na gwiji wa zamani wa klabu hiyo Paul Scholes, Ambaye amekua akimkosoa mchezaji huyo mara kwa mara kutokana na uchezaji wake.

Mchezaji huyo amekua akionesha ufundi uwanjani wa kuchezea mpira huku yeye akiamini anadumisha utamaduni wa kwao Brazil, Na ndio umemfanya kuwepo alipo lakini wengine hawafurahishwi na anachokifanya mchezaji huyo.antonyHii imekua ikiwakumba wachezaji wengi wanaotoka Brazil, Kwani hata Neymar ameshawahi kukosolewa kutokana na aina yake ya uchezaji lakini na yeye pia alisisitiza hawezi kuacha utamaduni wao.

Acha ujumbe