Barcelona wamethibitisha kuwa Ronald Araujo alipata jeraha la paja alipokuwa kwenye majukumu ya Kitaifa na Uruguay, na kuongeza orodha ya majeruhi katika safu ya ulinzi ya Barca baada ya Kounde kupata jeraha la misuli ya paja.

 

Araujo Aongezeka kwenye Orodha ya Majeruhi

Araujo alifanyiwa mabadiliko dakika tano tuu baada ya Uruguay kupoteza 1-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Iran nchini Austria siku ya Ijumaa, ambapo mapema siku ya Ijumaa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa lilimtangaza Jules Kounde kuondoka kwenye kikosi cha Didier Deschamps baada ya kufanyiwa mabadiliko wakati wa ushindi wao wa ligi ya Mataifa dhidi ya Austria siku ya Alhamisi.

Barcelona mpaka sasa wameweka wazi  hali ya majeruhi hao wawili, huku Araujo akipata mvunjiko katika paja la kulia, huku Kounde akipata jeraha katika msuli wake wa kushoto, ambapo taarifa rasmi kutoka kwa Barca kuwa lini beki huyo atarejea haijawekwa bayana, lakini taarifa kutoka nchini Uhispania zinasema wote wawili kuwa wanaweza kuwa nje ya uwanja takribani mwezi mmoja.

 

Araujo Aongezeka kwenye Orodha ya Majeruhi

Kuwakosa wachezaji hao wote wawili kwa wakati mmoja, itakuwa pigo kubwa kwa Xhavi, ambaye amewafanya wawili hao kuwa nguzo kuu za ulinzi katika timu yake mpya.

Araujo ameanza mechi sita zote za Barca kwenye Laliga msimu hu, wakati Kounde ambaye amejaza nafasi ya beki tangu ahamishwe kutoka Sevilla ametoa assist mbili katika mechi tatu za Ligi kwa wababe hao wa Camp Nou.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa