Usiempenda ndio kauli ambayo unaweza kusema baada ya droo ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kuchezeshwa na moja ya mechi za robo fainali itakutanisha vilabu vya Arsenal dhidi ya Fc Bayern Munich.
Arsenal waliokua kwenye ubora mkubwa sana kwasasa wanakwenda kukutana na Bayern Munich ambayo inaonekana kuchechemea, Lakini vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza wana kumbukumbu mbaya dhidi ya miamba hiyo ya soka kutoka nchini Ujerumani.Baada ya Arsenal kutoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa takribani misimu saba, Hatimae wamerudi mwaka na wanakwenda kukutana na timu ambayo iliwatoa kwa mara ya mwisho kwenye michuano hiyo kwa fedheha baada ya kufungwa mabao 10-2 kwenye michezo miwili.
Klabu ya Arsenal msimu wanaonekana wako kwenye ubora mkubwa sana wakitoa ushawishi kua wanaweza kulipa kisasi kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya soka ya Ujermani Bundesliga.Klabu ya Fc Bayern Munich licha kutokua na mwendelezo mzuri katika michezo yao msimu huu, Lakini ni moja ya timu zenye uzoefu mkubwa kwenye michuano hiyo na inaweza kushinda mchezo huo licha ya kutokua kwenye ubora wao.