Arsenal Karibu Zaidi na Saini ya Tiago Tomas

Arsenal wameripotiwa kuwa karibu zaidi na kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Sporting Lisbon Tiago Tomas kwa mkataba wenye thamani ya pauni milioni 20.

Mchezaji huyo wa miaka 18 alifanikiwa kuingia kikosi cha kwanza kwa miamba wa Ureno msimu huu na amecheza mara kwa mara kwa upande timu yake ikifanya poa na kuwa kileleni mwa jedwali la Primeira Liga.

Kwa mujibu wa The Sun, mkurugenzi wa michezo Edu amekuwa akiwasiliana moja kwa moja na mkurugenzi wa mpira wa miguu Hugo Viana juu ya mpango wa kumsaini Tomas wakati akimfuatilia fowadi huyo kwenye mechi yao dhidi ya Benfica, ambao Gunners watakutana nao kwenye Ligi ya Europa Alhamisi ijayo.

Arsenal Karibu Zaidi na Saini ya Tiago Tomas

Kijana huyo hivi karibuni alisaini kandarasi mpya, ilikuwa Juni 2020, kandarasi inajumuisha kifungu cha kununuliwa kwa mkataba kwa thamani ya pauni milioni 52.

Hata hivyo, kwa sababu ya hali ya kifedha ya sasa na matumizi ya Sporting kwa miaka michache iliyopita, inaeleweka kuwa kilabu hii ya Ureno inaweza kukubali dau la chini ya £20m.

Edu pia ameuambia uongozi wa Arsenal kwamba anaamini kilabu itajuta kumkosa mchezaji huyo mahiri.

Tomas amecheza mara 25 kwenye mechi za mashindano yote hadi sasa msimu huu, akifunga mabao matano na kutoa asisti tatu.

 


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

15 Komentara

    Safi Sana arsenal mmefanya vyema

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Arsenal yuko vizuri

    Jibu

    Vizur sana Arsenal

    Jibu

    Safi sana Arsenal

    Jibu

    Habar nzur hii

    Jibu

    Vizuri sana Arsenal

    Jibu

    Asante kwa taalifa

    Jibu

    Tatizo la Arsenal si kusajiri bali ni zaidi ya hapo

    Jibu

    Habari ikopoa

    Jibu

    Arsenal wametisha kinyamaaa

    Jibu

    Habari nzuri kwa Arsenal

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Itakuwa poa

    Jibu

Acha ujumbe