Arsenal Kuachana na Kiwior

Klabu ya Arsenal wana uwezekano mkubwa wakaachana na beki wake wa kushoto Jakub Kiwior kama watapata ofa nzuri kwa klabu yeyote ambayo itahitaji kumnunua beki huyo.

Raia huyo wa kimataifa wa Poland amejiunga na klabu ya Arsenal mwaka jana mpaka sasa ameitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja na nusu , Washika mitutu hao wa London wanataka kuachana nae kutokana na kutoridhishw ana uwezo ambao ameuonesha beki huyo ndani ya viunga vya Emirates.ArsenalSababu kubwa itakayomuondoa Kiwior ndani ya klabu ya Arsenal imeelezwa ni ujio wa beki raia wa kimataifa wa Italia Riccardo Calafiori ambaye anacheza nafasi moja na beki huyo wa kimataifa wa Poland, Kama dili la Calafiori litakamilika ni wazi Kiwior hatakua na nafasi ndani kikosi cha kocha Mikel Arteta.

Washika mitutu wa London wanaelezwa kama klabu zitashindwa kumnunua kwenye dirisha hili basi wataruhusu mchezaji huyo aondoke kwa mkopo, Lakini sharti litakua moja kwa klabu ambayo itamuhitaji kwa mkopo na sharti lenyewe ihakikishe inamnunua beki huyo wa kimataifa wa Poland.ArsenalVilabu mbalimbali kutoka nchini Italia vinaelezwa kufatilia kwa karibu hali inayoendelea baina ya klabu ya Arsenal na beki Jakub Kiwior, Hivo kuna uwezekano vilabu hivyo vikapeleka ofa na kama ilivyoelezwa hapo mwanzo kwa klabu yeyote ambayo itafikia ofa ambayo Washika mitutu hao London wameiweka basi klabu hiyo itamuachia Kiwior.

Acha ujumbe