Arsenal Kudaka Mmoja wa Salzburg

Hivi juzi wakati wa mechi nzito kati ya Chile na Uruguay kulitokea kioja kikubwa kwa mchezaji mkubwa kama Suarez kutaka kufanya udanganyifu uwanjani kwa kumshawishi muamuzi kuita mpira wa penati baada ya mlinda mlango kudaka mpira akiwa katika eneo lake; jambo hilo lilikuwa la ajabu sana katika soka.

Baada ya kioja hicho tuangazie pazia la usajili linaendeleaje katika klabu mbalimbali:

Mipango ya Perez juu ya James Rodriguez, inasemekana tajiri huyo wa Madrid ana mpango ambao ameusuka vizuri kuhusu mchezaji huyo kumuuza Napoli. Anaangazia jicho lake kuifanya biashara hiyo wakati mashindano ya upande huo wa bara la Amerika Kusini yakiwa yanaendelea na kutumia kiwango cha nyota huyo katika mashindano hayo kama chambo cha biashara. Hii ni kulipa kama ilivyotokea kwake wakati alipomnunua kwa kuangalia uwezo wake kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014.

Spurs waangazia jicho lao kwa Andreas Skov Olsen, nyota huyo mwenye makali yake na raia wa Denmark amekuwa katika mipango ya kuangaliwa sana na klabu hiyo ambayo imevutiwa na uwezo wake kwa kuona kwamba anaweza kuwa sehemu nzuri sana ndani ya kikosi hicho kwa kumpa nafasi zaidi kwenye soko lao la usajili la msimu huu. Nyota huyo ambaye bado umri wake unaruhusu kuwa sokoni kwa hakika atawafaa sana.

Dominik Szoboszlai wa Salzburg anaweza kutua Arsenal, mchezaji huyo amekuwa msaada mkubwa katika klabu yake hiyo na anategemewa kuwa katika kikosi cha Washika Bunduki kwa siku zijazo kama makubaliano baina ya pande hizo mbili yatakwenda sawa. Nyota huyo anaangaliwa kuwa atakuja kuwa katika kiwango cha juu sana na atakuwa kati ya viungo bora sana ndani ya soka.

United warudisha majeshi yao kwa Jadon Sancho, ripoti zinaeleza kwamba klabu hiyo ya matajiri hao wa jiji la Manchester wamerudi upya sokoni kutaka kumfukuzia nyota huyo raia wa Uingereza ambaye alikuwa na msimu mzuri sana na Dortmund. Na wameamua kuanza mazungumzo upya baada ya wachezaji wake wawili kuwa katika dalili za kuondoka klabuni hapo hivyo wapo kuangalia mbadala wao na Sancho ataweza kuwafaa.

Semedo anaviziwa na PSG, baada ya kupata taarifa kwamba nyota wao na mlinzi ndani ya klabu hiyo, Alves hatoongeza mkataba wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ufaransa pia mlinzi wao, Thomas Meunier kuonekana kuwa katika hali ya kusita kuongeza kandarasi yake basi klabu hiyo imemuweka kwenye rekodi zake mlinzi huyo wa Barcelona kwenye mipango yake ili kuweza kuona kama watamnasa mapema.

2 Komentara

    Refarii wawe makini sana na suarez mana ndozake.

    Jibu

    Habar njema kwa mashabik wa gunners

    Jibu

Acha ujumbe