Klabu ya Arsenal imekubali kumnunua kwa uhamisho wa kudumu golikipa David Raya ambaye yupo kwa mkopo klabuni hapo akitokea klabu ya Brentford inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Klabu ya Brentford ilikubali kumuachia kwa mkopo golikipa wake namba moja David Raya kwenda klabu ya Arsenal kwenye dirisha kubwa lililopita, Ambapo Arsenal wamekubali kumnunua kwa uhamisho wa kudumu golikipa huyo.Golikipa huyo yupo klabuni hapo kwa mkopo wa msimu mzima yaani mkataba wake unamalizika Juni mwaka 2024, Huku Washika bunduki kutoka London nao wamepanga kumnunua jumla mwezi Juni mwaka 2024.
Paundi milioni 27 ndio itatumika kumsajili David Raya kwa uhamisho wa kudumu kujiunga na washika mitutu hao wa London katika dirisha kubwa la mwezi wa sita mwaka 2024.Arsenal wameepuka kulipa kiwango cha pesa katika dirisha dogo kwa Brentford kwajili ya kuepuka sheria za uwiano wa matumizi ya pesa ambayo yanafanya vilabu vingi kufungiwa, Ikiwa ndio sababu ya kulipa kiasi hicho katika dirisha kubwa mwakani.