Klabu ya Arsenal itaingia sokoni kwenye dirisha dogo la mwezi Januari kutafuta mshambuliaji na mipango yao ipo kwa mshambuliaji wa klabu ya Juventus Dusan Vlahovic.
Arsenal wamekua wakimvia mshambuliaji Dusan Vlahovic kwa muda mrefu lakini hawakufanikiwa kumpata, Huku mshambuliaji akielekea klabu ya Juventus kwneye dirisha dogo msimu uliomalizika.Washika mitutu hao wa London wanahitaji mshambuliaji mwenye ubora mkubwa wakiamini ndio sababu itakayoweza kuwapa nafasi kutwaa ubingwa, Kwani mshambuliaji wao namba moja Gabriel Jesus amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara.
Klabu ya Juventus inaelezwa ipo tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa zamani wa Fiorentina, Lakini sharti ni moja tu kwa klabu ambayo itafika kiwango cha pesa ambacho mabingwa hao wa zamani wa Italia wamekiweka.Klabu ya Arsenal hawatakua wenyewe kwenye mbio za kumuwania mshambuliaji Dusan Vlahovic, Kwani vigogo wa soka kutoka nchini Hispania klabu ya Real Madrid wanaelezwa na wao wanahitaji saini ya mshambuliaji huyo raia wa kimataifa Serbia.