Klabu ya Arsenal ina mpango wa kurudi kwa kiungo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Aston Villa kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Arsenal wanaelezwa wanataka kutuma ofa kwa kiungo huyo katika dirisha la mwezi Januari ili kuhakikisha wanaimarisha eneo lao la kiungo ambalo linaonekana kuandamwa na majeraha.arsenalWashika mitutu hao wa London wanataka saini ya Luiz kutokana na kiungo wao Thomas Partey mara nyingi kuandamwa na majeraha, Hivo kuja kwa kiungo wa kimataifa wa Brazil kutawasaidia kwa kiwango kikubwa.

Kiungo Douglas Luiz amekua na kiwango kizuri sana ndani ya klabu ya Aston Villa, Jambo ambalo limewafanya washika mitutu kuhitaji saini yake wakiamini atakuja kuongeza ubora kwenye kikosi hicho.arsenalHii inakua sio mara ya kwanza kwa klabu ya Arsenal kufukuzia huduma ya Douglas Luiz, Kwani msimu uliomalizika kwenye dirisha dogo la mwezi Januari pia walikaribia kunasa huduma ya kiungo huyo lakini Aston Villa wakaweka ugumu na kumpa kiungo huyo mkataba mpya.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa