Arsenal na Chelsea Vitani kwa Calafiori

Vilabu viwili kutoka jijini Arsenal, na Chelsea wameingia vitani kuwinda saini ya beki wa kimataifa wa Italia ambaye anakipiga klabu ya Bologna inayoshiriki ligi kuu nchini Italia.

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta inaelezwa amekubali Calafiori kua moja ya mipango ya mabeki wake msimu ujao na bajeti ambayo imewekwa mezani ni kiasi €milini 50, Lakini mpaka sasa washika mitutu hao wa London hawajatuma ofa rasmi ndani ya klabu ya Bologna.arsenalKlabu ya Chelsea nao wanaelezwa kutafuta beki wa kati katika dirisha hili kubwa baada ya mabeki wake wengi wa kati klabuni hapo kutokua na ubora ambao ulitarajiwa, Lakini pia kuondoka kwa beki mkongwe klabuni hapo ambaye alikua anaisaidia klabu hiyo kwa kiwnago kikubwa Thiago Silva.

Vita ni kubwa baina ya vilabu hivo viwili kutoka jiji la London kwakua wote wanamuhitaji  beki huyo wa kimataifa Italia kutokana na mahitaji ya vilabu vyote viwili, Lakini mpaka sasa hakuna klabu yeyote ambayo imetuma ofa rasmi kati ya vilabu hivyo viwili.arsenalKlabu ya Arsenal mpaka sasa wanaonekana wanaweza kua na faida zaidi kwakua wana mahusiano mazuri baina yao na klabu ya Bologna kwakuwa wameshafanya biashara baina yao kwa Takehiro Tomiyasu, Lakini mbali na hapo vilabu hivo kutoka London vitakutana na upinzani mkali kutoka klabu ya Juventus.

Acha ujumbe