Arsenal na Havertz Mambo ni Shwari

Klabu ya Arsenal imekaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz alieykua anakipiga katika klabu ya Chelsea kwa usajili wa Euro milioni 65.

Arsenal inapambana kuhakikisha inafanya maboresho kueleka msimu ujao wa ligi kuu ya Uingereza, Huku moja ya sajili ambazo zinakuja kuongeza chachu kwenye kikosi cha Washika mitutu hao wa London ni Kai Havertz.ArsenalKiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani alikua na msimu bora ndani ya klabu ya Chelsea mwaka 2021, Lakini misimu ya hivi karibuni ameonekana kushuka ubora lakini kocha Arteta amemuhitaji kwenye timu yake kwakua anaamini ubora wake.

Wakati Arsenal wanakamilisha usajili wa Kai Havertz pia wako kwenye hatua za mwisho katika usajili wa kiungo wa klabu ya West Ham United na hii inaonesha ni kwa namna gani klabu hiyo imeupania msimu ujao kwani wanafanya usajili kwa umakini mkubwa.ArsenalArsenal chini ya Mikel Arteta imeonekana kubadilika sana na kuboresha ubora wa kikosi hicho ndani ya misimu mitatu aliyokaa klabuni hapo, Hii imedhihirika msimu uliomalizka ambapo walimaliza nafasi ya pili kitu ambacho hakuna aliyetarajia

Acha ujumbe