Klabu ya Arsenal nayo itaingia kwenye mbio za kumuwania mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe ambaye ametangaza kuondoka ndani ya klabu yake ya PSG mwisho wa msimu.
Wakati kocha wa Arsenal akifanya mazungumzo leo na wanahabari aligusiwa na wanahabari juu ya uwezekano wa kumsajili Mbappe na majibu yake yalikua kama hivi “Kwanini tusiingie kwenye mazungumzo nae, Kama tunataka kua bora tunahitaji wachezaji wenye vipaji vikubwa na wachezaji wakubwa”Kocha huyo pia aliendelea kwa kusema “Lakini sipo kwenye mazungumzo labda Edu na mmiliki wa klabu, Sitakuwepo kwenye mazungumzo mpaka kwenye hatua za mwisho” Hayo ndio yalikua majibu ya Arteta.
Kocha huyo ameonesha kua klabu hiyo inaweza kuingia pia kwenye kinyang’anyiro cha kumuwania mchezaji huyo ambaye ni moja ya wachezaji bora kwasasa duniani kwakua kama wanataka kua timu bora wanapaswa kua na wachezaji bora.Taarifa zinaeleza kwa kiwango kikubwa kua mchezaji Kylian Mbappe anaweza kwenda Real Madrid, Lakini hakuna uhakika wa aslimia 100 hivo Arsenal nao wanaingia kwenye mbio za kumuwania mchezaji huyo mpaka pale ambapo itafahamika ni nani atashinda mbio hizo.