Arsenal Waipasua Spurs North London Derby Waweka Rekodi

Klabu ya Arsenal wamefanikiwa kuifunga klabu ya Tottenham Hotspurs wakiwa ugenini katika dimba la Spurs kwa bao moja kwa bila ambalo limefanikiwa kuwapa alama tatu muhimu wakiwa ugenini.

Klabu ya Arsenal ambao walianza mchezo kwa kiwango kikubwa wakionekana wako nyuma zaidi na Tottenham wakionekana kutawala zaidi mchezo huo, Lakini matomeo yaliisha kwa washika mitutu wa London kuibuka na ushindi tena wakiwa ugenini.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana huku Spurs wakionekana kutawala zaidi mchezo, Lakini kipindi cha pili kilikua tofauti kwani vijana wa Mikel Arteta walionekana kufanya mashambulizi ya kushtukiza mara kwa mara Spurs walipokua wanapoteza mpira.arsenalNi beki Gabriel ambaye aliwaeka washika mitutu mbele mnamo dakika ya 64 ya mchezo baada ya kumalizia vizuri mpira wa kona ambao ulipigw na winga Bukayo Saka, Mchezo huo ulienda hivo mpaka dakika tisini za mchezo kumalizika na washika mitutu wa London kuibuka na ushindi.

Rekodi imewekwa Arsenal sasa wanafanikiwa kushinda michezo minne mfululizo katika North London Derby wakiwa ugenini tangu mwaka 1988, Hivo hii ni rekodi mpya kwao lakini pia klabu hiyo imefanikiwa kupata ushindi huo licha ya kuwakosa nyota wake wawili Martin Odegaard na Declan Rice.

Acha ujumbe