Arsenal Wajitoa kwa Lavia

Klabu ya Arsenal wanaripotiwa kuachana na mchakato wa kumnunua kiungo wa klabu ya Southampton Romeo Lavia huku Liverpool ikibaki kwenye mbio hizo.

Arsenal wanaelezwa kuachana na mpango wa kumsajili Romeo Lavia kutokana na mazungumzo chanya ambayo yameendelea na kiungo wa klabu hiyo Thomas Partey ambaye inasemekana ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo.arsenalKlabu ya Liverpool wao wamejiandaa kupeleka kiasi cha paundi milioni 42 kwa klabu ya Southampton kwajili ya kumsajili Romeo Lavia ambapo klabu ya Southampton wao wanahitaji kiasi cha paundi milioni 50 kama ambavyo walieleza hapo awali.

Liverpool wanataka kuhakiksha wanakamilisha dili la Romeo Lavia kwasababu kuna taarifa klabu ya Chelsea wamejiunga kwenye mbio za kumuhutaji kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji.arsenalArsenal wao mpaka sasa wameshatumia kiasi kikubwa cha pesa kwenye usajili ikiwa ni rekodi mpya kwa klabu hiyo, Hivo kiwango cha pesa kilichowekwa na klabu ya Southampton kimeonekana ni kikubwa kwa klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London.

Acha ujumbe