Arsenal wamepiga hatua kubwa kwa kufikia makubaliano ya awali kumsajili kiungo wa Brazil, Bruno Guimaraes, kutoka Newcastle United. Kwa mujibu wa Daily Mail, dili hili linakadiriwa kufikia pauni milioni 77 pamoja na bonasi na nyongeza zingine. Ingawa mikataba rasmi bado haijatiwa saini, usajili huu sasa uko hatua za mwisho na unakaribia kutangazwa.

Newcastle walipambana kwa nguvu kumzuia nyota wao wa miaka 28, hasa baada ya kupoteza majina makubwa kama Sandro Tonali na Anthony Gordon, pamoja na kujiuzulu kwa kocha Eddie Howe. Lakini msimamo wa Guimaraes ulikuwa wazi, alishatuma ujumbe kwa uongozi kwamba anataka kuondoka, na hata kukataa kusafiri na kikosi kwenda kambi ya mazoezi La Manga.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Guimaraes, mshindi wa Kombe la Ligi na Newcastle Machi 2025 na mshiriki wa fainali za Kombe la Dunia, anakuwa usajili wa nne wa Arsenal msimu huu. Kabla yake, Arsenal walikamilisha uhamisho wa beki Piero Hincapie kutoka Bayer Leverkusen, kumsajili kipa Illan Meslier bure, na kumnasa winga wa Kigiriki Christos Tzolis kutoka Club Brugge kwa pauni milioni 36.

Arsenal walikuwa wamejaribu kumsajili Guimaraes tangu 2022 alipokuwa Lyon, lakini Newcastle waliwapiku wakati huo. Sasa, baada ya miaka minne, Gunners wamefanikiwa kumaliza safari ya muda mrefu ya kumleta kiungo huyu Emirates.


