Arsenal Wamemlipa Auba £7M Kuondoka Emirate.

Ndani ya masaa machache, Januari 31, 2022 safari ya Arsenal na Pierre-Emerick Aubameyang ilifikia tamati. Miaka 4 imeisha tamatika.

Januari 31, 2018 Aubameyang alitua Emirate Stadium akitokea Borussia Dortmund. Januari 31, 2022, Aubameyang anaonekana uwanja wa ndege Barcelona, Uhispania kuashiria mwisho wa safari yake na Arsenal baada ya miaka 4.

Haikuwa rahisi. Ni mwishoni mwa msimu uliopita, Aubameyang alisani mkataba mpya na The Gunners na kuondoa habari za kuondoka klabuni hapo. Msimu huu umekuwa wenye visa na matukio ya kila namna – ndani na nje ya uwanja.

Kushuka kwa kiwango uwanjani, masuala ya kinidhamu yakamuondolea unahodha na kisha, mpaka anaondoka Emirate, alikuwa na takribani wiki 7 hatumiki kwenye kikosi cha Mikel Arteta.

Mwisho wa siku, sintofahamu na mvutano kati yake na Arteta umefikia mwishoni. Auba ameondoka Emirate kwa maridhiano kati yake na uongozi wa klabu hiyo. Alikuwa amebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake ambapo pia, alikuwa analipwa £350,000 kwa wiki.

https://www.instagram.com/reel/CZcg2udpg1C/?utm_source=ig_web_copy_link

 

Kuachana kwa pande hizi, hakujatokea kirahisi tu. Gharama zimehusika. Inaripotiwa kuwa, Arsenal wamemlipa Aubameyang takribani £7M ili kusitisha mkataba wake na kuondoka kama mchezaji huru.

Kama klabu, wameshatoa tamko la kuthibitisha kuondoka kwa Auba. Vivyo hivyo, Auba ameweka chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwashukuru mashabiki wa klabu hiyo na kuitakia kheri timu hiyo.

https://www.instagram.com/p/CZc2wOlt1ZF/?utm_source=ig_web_copy_link

Barcelona kwa upande wao, bado hawajatoa uthibitisho rasmi wa usajili wa Auba japokuwa, raisi wa klabu hiyo amesema wazi, mchakato wa kukamilisha usajili unakwenda vizuri na, mchezaji huyo ameshaanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa FC Barcelona.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe