Klabu ya Arsenal inaripotiwa kuwa inafikiria kumsainisha mkataba mpya mlinzi wao mwenye uzoefu mkubwa David Luiz.
Mkataba wa sasa wa nyota huyu mwenye miaka 34 kuendelea kuwepo dimbani Emirates unafika tamati mwezi Juni, huku uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya staa huyu ukitarajiwa kuwa utasubiri 2020-21.
Lakini kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Brazil, Arsenal wanapima maamuzi yao ikiwa ni sahihi kumuongezea mkataba beki huyu kuendelea kuwepo hadi angalau Juni 2022.
Hata hivyo, staa huyu pia amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa wakiwemo Benfica and Fenerbahce, wote wakiwa wanafuatilia kwa ukaribu muenendo wa hatma ya mkataba wake.
Luiz amekuwa na kipindi kigumu akipata majeraha kadhaa msimu huu, lakini amecheza kwenye mechi 30 za michuano yote msimu huu chini ya Mikel Arteta, akifanikiwa kuona lango mara 2.
Mlinzi huyu alishindwa kuwepo kwenye kikosi chake dhidi ya Villareal katika mechi ya pili ya nusu fainali ya Ligi ya Europa akiwa na jeraha la pajha.
TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO
Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!
Jamani mpeni mkataba yuko vizuri tu#meridianbett
Nice
Wamwongezee tu mkataba yuko vizuri
Good news
Asante kwa [email protected]
Jamaa yupo vizuri
Good
Safii
Wamuingezee tu muda
Jamahaa najua uyo
Wamuache Tu galasa ilo
Nice