Klabu ya Arsenal ambayo kocha wake mkuu ni Mikel Arteta wameanza vizuri michuano ya Europa League vizuri baada ya kupata ushindi wao kwenye mechi ya kwanza ambapo walikuwa wakicheza dhidi ya FC Zuerich.

 

Arsenal Yaanza Vizuri Europa

Arsenal walikuwa ni wageni wa timu hiyo ambaye makao makuu yake ni Switzerland ambapo The Gunners alishinda kwa bao 2-1, mabao hayo yalitupiwa kimyani na Marquinhos pamoja na Nketiah wakati kwa upande wa Zuerich bao lao  lilifungwa na Kryeziu na mchezo kumalizika wa The Gunners kuibuka washindi.

Arsenal mchezo unaofata kwenye michuano hii ya Europa watakutana na Psv ambao wao wametoka kuapata sare ya 1-1 dhidi ya Bodoe/Glimit. Kabla ya kuvaana na Psv vijana wa Arteta watacheza na Everton katika mechi yao nyingine ya mzunguko wa saba kwenye Epl.

 

Arsenal Yaanza Vizuri Europa

Mchezo uliopita wametoka kupoteza dhidi ya Manchester United kwa mabao matatu kwa moja lakini bado wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama moja katika yao na aliye nafasi ya pili  ambayo inashikiliwa na Manchester City.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa