Arsenal Yafunga Dili la £50M Kumsajili Ezri Konsa

Arsenal imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kati wa Aston Villa, Ezri Konsa, katika dili lenye thamani ya £50 milioni kama ada ya awali pamoja na nyongeza. Mikel Arteta amefanikiwa kumpata mmoja wa mabeki anayejua vizuri soka la England, huku usajili huo ukitarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal.

Arsenal Yafunga Dili la £50M Kumsajili Ezri Konsa

Konsa, ambaye ni raia wa England, amekubali masharti binafsi ya mkataba baada ya Arsenal kufikia makubaliano na wawakilishi wake. Hilo limeondoa kikwazo kikubwa katika uhamisho huo, huku pande zote zikielekea kukamilisha hatua za mwisho za dili hilo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Arsenal Yafunga Dili la £50M Kumsajili Ezri Konsa

Arteta amekuwa akimtaka Konsa kama sehemu ya mipango yake ya kuimarisha kikosi, hasa kwenye eneo la ulinzi. Uwezo wake wa kucheza kama beki wa kati unatarajiwa kumpa Arteta chaguo zaidi ndani ya kikosi, huku akiongeza ushindani kwenye safu ya nyuma ya The Gunners.

Arsenal Yafunga Dili la £50M Kumsajili Ezri Konsa

Kwa Aston Villa, kuondoka kwa Konsa kungekuwa pigo kwenye safu yao ya ulinzi, lakini ada ya £50M pamoja na nyongeza inaweza kuwa sehemu muhimu ya mipango yao ya kujenga upya kikosi. Kwa upande wa Arsenal, hii ni hatua nyingine kubwa katika harakati za Arteta kuunda kikosi chenye uwezo wa kupigania mataji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.