Taarifa za uhakika ni kuwa Klabu ya Arsenal imekamilisha mchakato wa kumsajili Gabriel Jesus kwa ada ya Paundi Milioni 45 na tayari majadiliano kuhusu mahitaji binafsi ya mchezaji yamefikiwa.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City amekuwa akiwaniwa na Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kwa muda, ikielezwa kuwa Jesus amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano.

 

Gabriel Jesus
Gabriel Jesus

Jesus anatarajia kutua London akitokea kwao Brazil kwaajili ya kukamilisha usajili na kufanyiwa vipimo vya afya wiki hii baada ya makubaliano kufikiwa baina ya vilabu hivyo viwili.

Jesus anatua Arsenal kuziba nafasi ya ushambuliaji iliyoachwa wazi na mshambuliaji wa Gabon, Aubameyang na yule wa Ufaransa, Lacazette aliondoka majira haya ya kiangazi.

Manchester City inaweza kutumia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Leeds United, Kalvin Phillips ambaye amekubali kutua Etihad kwa dau la Paundi Milioni 42.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa