Klabu ya Arsenal imefanikiwa kumuongeza mkataba kiungo wake wa kimataifa wa Misri Mohamed Elneny mkataba ambao utaendelea kumueka kwenye viunga vya Emirates mpaka mwezi Juni 2024.

Arsenal imemuongozea mkataba kiungo huyo ambaye mkataba wake ulikua unamalizika mwishoni mwa msimu huu, Washika mitutu hao wa London wameamua kumuongezea kiungo huyo mkataba kwajili ya kuendelea kuimarisha eneo lao la katikati Elneny akiendelea kushirikiana na Partey, Odegaard, Xaka, na Jorginho.ArsenalArsenal wamekua na utaratibu wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu siku za karibuni na huo umekua mpango wa kocha Mikel Arteta ambaye ameeleza anawaongezea mikataba wachezaji wake muhimu ambao wapo kwenye mipango yake.

Mohamed Elneny amekua mchezaji ambaye haanzi kwenye michezo mingi ndani ya klabu hiyo lakini mpaka ameongezewa mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo ni wazi mchezaji ambaye yupo kwenye mipango ya kocha Mikel Arteta.ArsenalArsenal mpaka sasa wamefanikiwa kuwaongeza mkataba wachezaji kama Gabriel Martinelli, Gabriel Malgahes, na Mohamed Elneny mpaka sasa klabu hiyo inapambana kumuongezea mkataba mpya mchezaji anayefanya vizuri zaidi klabuni hapo kwasasa Bukayo Saka ambaye wapo kwenye mazungumzo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa