Klabu ya Arsenal imefanikiwa kupiga comeback ya kibabe dhidi ya klabu ya Bournamouth katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Emirates na kushuhudia washika mitutu hao wa London wakishinda mabao matatu kwa mawili.
Klabu ya Arsenal ilitanguliwa na Bournamouth kwa goli la mapema dakika ya kwanza ya mchezo bao likifungwa na Philip Billing, Mchezo huo uliendelea kwa washika mitutu kujaribu kusawazisha bao katika mchezo huo lakini mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Bournamouth walikua mbele kwa bao moja.Kipindi cha pili kilianza kwa vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza wakijitahidi kuhakikisha wanawazisha bao hilo, Lakini kabla hawajasawazisha Bournamouth walifanikiwa kupata bao la pili kupitia mpira wa kona goli lililofungwa na beki Marcos Senesi.
Klabu ya Arsenal waliendelea kucheza kwa utulivu ili kusawazisha mabao ambayo walitanguliwa dakika ya 62 ya mchezo klabu hiyo ilipata bao la kwanza kupitia kwa kiungo Thomas Partey, Kabla ya beki Ben White kuisawazishia klabu hiyo bao la pili mnamo dakiika ya 70 ya mchezo na ubao kusoma mabao mawili kwa mawili.Klabu ya Arsenal ilikamilisha comeback yake baada ya kumalizika kwa dakika 90 na kuongezwa dakika 6, Reis Nelson dakika ya 97 ya mchezo aliweza kuwapatia washika mitutu bao la tatu na kufanikiwa kushinda mchezo huku wakifikisha alama 63 wakiendelea kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.