Arsenal Yapigwa na Newcastle

Arsenal mambo yanaendelea kuonekana kua magumu ndani ya msimu huu kwani mpaka sasa wahsapokea vipigi viwili na sare michezo mitatu, Hii imekuja baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya Newcastle leo.

Arsenal wanaonekana kuanza msimu huu kitofauti kwani wameonekana kutokua kwenye ubora wao tofauti na misimu miwili iliyopita ambayo walionekana kua timu ngumu kwelikweli, Lakini mpaka sasa msimu huu tayari wameshakubali kudondosha alama 12 kati ya 30 mpaka sasa.arsenalMchezo dhidi ya Newcastle washika mitutu walionekana kucheza kwa tahadhari kipindi cha kwanza na kuwaacha wenyeji kutawala mchezo jambo ambalo lilipelekea madhara langoni mwao na kuruhusu goli kupitia kwa mshammbuliaji Alexander Isak mapema dakika ya 12 na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko vijana wa Mikel Arteta wakiwa nyuma.

Kipindi cha Arsenal walionekana kushambulia kwa kiwngo kikubwa wakihitaji kusawazisha goli walilotanguliwa na pengine kuongeza, Lakini safu ya ulinzi ya Newcastle ilionekana kua imara na mchezo kumalizika wakiwa wamepoteza kwa goli moja kwa bila ukiwa ni mchezo wao wa pili kupoteza.

Acha ujumbe