Arsenal Yapindua Meza Kibabe

Klabu ya Arsenal kwa siku nyingine imeshinda mchezo kibabe kwa kutokea nyuma kwenye mchezo ambao walikua nyuma dhidi ya klabu ya Southampton katika dimba la Emirates.

Arsenal walikua nyumbani leo wakiwakaribisha klabu ya Southampton ambapo walikua wanatawala mchezo huo toka dakika ya kwanza lakini hakufanikiwa kupata goli mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Hiyo ikitokana na umahiri wa klabu ya Southampton ambao waliuonesha kwenye kuzuia.arsenalKipindi cha pili kilianza kwa washika mitutu kutaka kupata goli baada ya kipindi cha kwanza kutoka bila goli lakini walishangazwa ambapo wageni ndio walikua wakwanza kupata goli kupitia Archer, Kabla ya Kai Havertz ksawazisha na baadae Gabriel Martinelli kuweka msumari wa pili na vijana wa Arteta kupata uongozi.

Wakati dakika zikiwa zinayoyoma winga Bukayo Saka alipiga msumari wa tatu na kuhakikisha meza imepinduka kibabe bila makandokando, Ambapo Arsenal sasa wanafikisha jumla ya alama 17 wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza nyuma ya Liverpool na Manchester City.

Acha ujumbe