Klabu ya Arsenal imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi wa mabao matatu kwa bila mbele ya klabu ya Brighton and Hove Albion.
Arsenal wakiwa ugenini wameweza kuendeleza fomu yao bora kabisa ambayo wamekua nayo msimu huu, Ambapo kuicharaza klabu ya Brighton wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.Vijana wa kocha Mikel Arteta walionekana kuingia kwa tahadhari kama ambavyo walianza dhidi ya Manchester City kwani Brighton ni moja ya timu ambazo zimekua na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira ndio sababu timu hiyo ilianza kwa tahadhari kubwa.
Dakika ya 33 ya mchezo klabu ya Arsenal walifanikiwa kupata mkwaju wa penati baada ya Gabriel Jesus kuchezewa madhambi kwenye eneo la hatari na mkwaju huo kuwekwa kambani na Bukayo Saka, Ambapo ilifanya ubao kusomeka bao moja kwa bila mpaka mchezo unakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kiliendelea kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku Brighton wakionekana kuhitaji kusawazisha bao ambalo wametanguliwa na Washika mitutu hao wa London, Lakini juhudi hazikuzaa matunda kwani ni vijana wa Arteta waliofanikiwa kupata goli la pili tena kupitia kwa Kai Harvertz dakika ya 62 ya mchezo.Arsenal walifanikiwa kuimaliza mechi kabisa baada ya kufunga bao la tatu kuoitia kwa winga Leandro Trossard ambaye alitokea nje kuchukua nafasi ya Gabriel Jesus na kufanya mchezo kumalizika kwa mabao matatu kwa bila, Huku Washika mitutu wa London wakienda kileleni baada ya kufikisha alama 71.