Klabu ya Arsenal imefanikiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga klabu ya Brentford katika dimba lao la nyumbani kwa jumla ya mabao matatu kwa bila.

Wakiwa ugenini washika mitutu hao wa London wameendelea kutakata baada ya kupata ushindi huo mnono wa goli tatu kwa bila magoli ya Gabriel Jesus,William Saliba pamoja Fabio Viera na kuwafanya timu hiyo kurudi kwenye nafasi yao ambayo wamekaa tangu ligi imeanza na jana ikikaliwa na klabu ya Manchester City kwa muda mchache kabla ya Arsenal kurudi kileleni na alama zao 18 wakifuatiwa na City wenye alama 17 katik msimamo wa ligi hiyo nchini Uingereza.

arsenalArsenal wanashinda mchezo wao wa sita wa ligi hiyo katika ya michezo saba waliyoshuka kiwanjani katika ligi hiyo ikiwa rekodi nzuri zaidi baada ya miaka mingi zaidi huku wakipoteza mchezo mmoja dhidi ya klabu ya Manchester United.

Mchezo huo pia uliwapa fursa pia wachezaji kama Thomas Partey na Kieran Tienery waliotoka katika majeraha na kurudi dimbani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa