Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ameonesha kuvutiwa na kiwango cha beki wake wa kulia raia wa kimataifa wa Uingereza Ben White na kuamua kumpa maua yake hadharani.
Kocha Mikel Arteta akiongea na wanahabari jana amempakulia minyama beki wake huyo wa kulia ndani ya kikosi hicho washika mitutu, Kwani ni wazi beki huyo amekua na kiwnago bora na kuendelea kuimarika siku hadi siku.“Ben typo tayari kujifunza kila siku, Kucheza kwenye hali yeyote akiwa anajiskia vizuri na hata wakati ambao hajiskii vizuri, Ni mtu ambaye akili yake imefunguka na anataka kushinda kila wakati na ndio kinacholeta utofauti kwake”
Kocha huyo ameamua kumpa sifa beki huyo kwani ni kweli beki Ben White ambaye alisajiliwa klabuni hapo kama beki wa kati, Lakini alipelekwa kucheza kama beki wa kulia ambayo ilikua nafasi ngeni kwake ila amefanikiwa kuonesha ubora mkubwa sana na kuendelea kuboresha uwezo wake kila siku.Kocha Mikel Arteta alipendekeza beki Ben White aongezewe mkataba na hii haikuja kwa bahati mbaya, Bali imetokana na uwezo ambao amekua akiuonesha beki ndani ya klabu hiyo ambapo amefanikiwa kua sehemu ya mabeki waliotengeneza ukuta mgumu zaidi kwneye ligi kuu ya Uingereza msimu ndani ya kikosi cha Arsenal.