Arteta Amsifu Kinda wake Nwaneri

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ampakulia minyama kiungo kinda wa klabu hiyo Ethan Nwaneri (17) ambaye amepata nafasi kwenye mchezo wa kombe la EFL jana na kuonesha kiwango kizuri.

Kinda Ethan Nwaneri jana ameonesha kiwango bora sana ambapo alifanikiwa kufunga mabao mawili katika mchezo ambao Arsenal walishinda kwa mabao matano kwa moja walioupata dhidi ya klabu ya Bolton Wanderers, Jambo lilimfanya kocha Mikel Arteta kukoshwa na kiwnago cha kijana huyo na kummwagia sifa.arteta“Anacheza bila shinikizo, kwa kujiamini, na kwa namna ya kufanya maamuzi inayoonyesha kwamba kijana yupo tayari kwenye kiwango hiki.”

“Yeye ni sehemu yetu kwa hivyo atapata dakika za kucheza. Anazidi kuboreka kila siku.”

Kijana huyo mwenye umri wa miaka (17) tu mpaka sasa ameonesha anaweza kufanya makubwa siku za mbeleni kama atapata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha Arsenal, Kinachosubiriwa kwa hamu ndani ya kikosi hicho ni kijana huyo aendelee kupewa nafasi na kocha Arteta aoneshe makubwa zaidi.

Acha ujumbe