Arteta Aonyesha Thamani Yake Zaidi Arsenal

Mikel Arteta amekuwa mhimili mkubwa wa mabadiliko ya Arsenal katika miaka ya hivi karibuni, huku takwimu zikionyesha kuwa mafanikio ya klabu hiyo yamekuwa makubwa zaidi ukilinganisha na kiwango cha fedha walichotumia kujenga kikosi. Kwa muda mrefu, soka limekuwa likijaribu kupata namna ya kutumia takwimu kueleza mambo yanayotokea uwanjani. Moja ya mambo yaliyoonekana wazi ni kwamba kiwango cha mishahara ya wachezaji mara nyingi kina uhusiano mkubwa na nafasi ambayo timu inaweza kumaliza katika ligi.

Arteta Aonyesha Thamani Yake Zaidi Arsenal

Ni jambo linaloeleweka kwa sababu katika ushindani wa soka, wachezaji bora mara nyingi hulipwa fedha nyingi zaidi. Hata hivyo, mshahara wa wachezaji hauwezi kueleza kila kitu, kwa sababu bado kuna nafasi kwa makocha bora kubadilisha kiwango cha timu zao.

Arteta anaonekana kuwa mmoja wa makocha hao. Mafanikio yake makubwa Arsenal yanaweza pia kuwa sababu ya mafanikio hayo kuonekana kama jambo la kawaida, wakati klabu hiyo imekuwa ikifanya vizuri zaidi ya inavyotarajiwa ukilinganisha na uwezo wake wa kifedha.

Katika misimu minne kati ya 2022/23 na 2025/26, Arsenal ilikusanya pointi nyingi zaidi za Premier League kuliko timu yoyote nyingine, ikifikisha pointi 332 dhidi ya 329 za Manchester City.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lakini jambo la kuvutia zaidi ni kwamba katika kipindi hicho Arsenal haikuwa klabu iliyokuwa na matumizi makubwa zaidi kwenye mishahara. Ilishika nafasi ya tano kwa ukubwa wa wage bill, ikimaanisha Arteta alikuwa akishindana na timu zilizokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kifedha.

Arteta Aonyesha Thamani Yake Zaidi Arsenal

Hata Arteta mwenyewe hakuwahi kuficha changamoto hizo. Januari 2025, alizungumza kuhusu “mapungufu fulani” yaliyokuwepo kwenye soko la usajili, akisema Arsenal ilikuwa imetoka mbali na matumizi yaliyokuwa yakifanywa na klabu nyingine.

Baadaye mwezi huo, Arteta alidai pia alikuwa na moja ya vikosi vyembamba zaidi kwenye ligi. Hata hivyo, Arsenal iliendelea kuongeza uwekezaji wake kila mwaka, hasa baada ya kuanza kujenga kikosi kipya chenye wachezaji vijana mwaka 2021.

Tatizo lilikuwa kwamba klabu nyingine za Premier League nazo zilikuwa zikiongeza matumizi kwa kasi. Hivyo, hata kama Arsenal iliongeza gharama za kikosi, haikuwa rahisi kuvuka pengo la kifedha lililokuwepo dhidi ya wapinzani wake.

Kwa sasa, Arsenal inatajwa kuwa na moja ya vikosi vyenye kina kikubwa zaidi Premier League, huku baadhi wakikiweka hata miongoni mwa bora barani Ulaya. Lakini Arteta hakujengewa kikosi hicho kwa kupewa fedha zisizo na kikomo.

Arteta Aonyesha Thamani Yake Zaidi Arsenal

Baada ya dirisha la usajili la majira ya joto kufungwa, gharama ya jumla ya kikosi cha Arsenal ilifikia takribani dola bilioni 1.15, lakini bado ilikuwa nafasi ya tano kwa gharama ya kikosi katika Premier League.

Hapo ndipo thamani ya Arteta inapojitokeza zaidi. Pamoja na usajili wenye akili na matumizi yaliyodhibitiwa, uwezo wake wa kufundisha na kuendeleza wachezaji umeisaidia Arsenal kuziba pengo ambalo lingeonekana wazi kwenye karatasi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.