Mikel Arteta ametwaa tuzo ya kocha bora wa Mwezi wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuwaongoza The Gunners kileleni kwenye msimamo mwezi August, huku akiwashinda Antonio Conte wa Tottenham Spurs, Graham Potter alipokuwa Brighton, na  Pep Guardiola wa Manchester City.

 

Arteta Atwaa Tuzo ya Kocha Bora

 

Arsenal walishinda mechi zao tano za kwanza za msimu wa ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya pili mwezi uliopita, baada ya kufanya hivyo hapo awali 2004-2005, na pia kujizolea sifa kwa mchezo wao wa kuvutia wa kumiliki mpira.

Vijana wa Arteta walikosa kufuzu michuano ya Klabu Bingwa msimu uliopita, Lakini wakaimarishwa na ujio wa Gabriel Jesus na Zinchenko ambao wameweka kasi zaidi kwenye kikosi. Ingawa The Gunners walifungwa 3-1 na United katika mechi yao ya kwanza ya mwezi Septemba na kushindwa kushinda mechi zao sita za mwanzo za ligi kuu tangu mwaka 1947-1948 .

 

Arteta Atwaa Tuzo ya Kocha Bora

Arteta sasa ameshinda Tuzo hiyo ya ukufunzi ya kila mwezi ya ligi kuu katika nyakati tatu tofauti Septemba 2021, pia Machi 2022 akilingana na Antonio Conte na Brendan Rodgers.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa