Kocha wa Mikel Arteta amekiri kuwa mchezaji wake Gabriel Jesus  atakuwa amesikitishwa sana hapo jana baada ya kukosa nafasi za kufunga mabao hapo jana kwenye mchezo dhidi ya Southampton.

 

Arteta: Jesus Amejisikia Vibaya Baada ya Kukosa Nafasi Hapo Jana.

The Gunners walikuwa waalikwa katika uwanja waSt Mary’s, huku washika mitutu hao wa London ndio walikuwa wa kwanza kupachik a bao kupitia kwa mchezaji wao Granit Xhaka katika dakika ya 11.

Xhaka amefunga mara ya pili mfululizo baada ya kufunga bao kwenye mchezo wao wa Uropa Alhamisi iliyopita na amaeafanya hivyo msimu huu akiwa na Arsenal. Gabriel Jesus anageweza kuendeleza alipoishia mechi zilizopita.

Mshambuliaji huyo wa Brazil licha ya kujaribu kupiga mashuti kibao lakini bado hakufanikiwa kupata bao ambalo labda lingewapa ushindi hapo jana ili waweze kuwakimbia mbali City.

Arteta: Jesus Amejisikia Vibaya Baada ya Kukosa Nafasi Hapo Jana.

Kocha wa Arsenal, Arteta alisema kuwa Jesus, alijaribu kupiga mashuti manne ya juu bila kumfunga golikipa wa Soton Bazunu, na hivyo huenda mechi ya jana itamfanya awe na hasira sana kutokana na kukosa mabao.

Baada ya sare ya hapo jana Arsenal wapo mbele  kwa pointi mbili dhidi ya Manchester City kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, ingawa uongozi huo ungeweza kuwa ni wa pointi nne endapo wangekuwa wameshinda mechi ya jana.

Arteta na vijana wake ndio kwanza wanapata sare ya kwanza msimu huu baada ya kucheza mechi 11 kwenye ligi huku wakiwa wameanza vizuri kampeni zao kwenye michuano yote msimu huu.

Arteta: Jesus Amejisikia Vibaya Baada ya Kukosa Nafasi Hapo Jana.

“Nadhani timu ilionekana safi mwanzoni,” Mhispania huyo aliongeza. “Niliiweka chini zaidi kwa jinsi tulivyocheza. Tulipaswa kucheza vizuri zaidi katika kipindi cha pili.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa