Mikel Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa uwepo wa mashabiki kwenye mchezo wao wa Europa League dhidi ya Rapid Wien ndani ya Uwanja wa Emirates umewapa nguvu kuibuka na ushindi huku mashabiki waliojitokeza wakitaka jina la Mesut Ozil kurejeshwa ndani ya timu hiyo.

Arteta, Arteta: Mashabiki ndio Chachu ya Ushindi, Meridianbet

Awali mashabiki walikuwa wamezuiwa kuingia ndani ya Uwanja kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona jana waliruhusiwa mashabiki 2,000 ambao waliingia na mabango yaliyoandikwa arejeshwe Ozil mwenye miaka 32 baada ya jina lake kutolewa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza ndani ya Ligi Kuu England pamoja na Eropa League.

Mabao ya Arsenal wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 yalifungwa na Alexandre Lacazette dk 10, Pablo Mari dk 18,Eddie Niketiah dk 44 na Emile Smith Rowe dk 66 lile la Rapid Wien lilipachikwa na Koya Kitagawa dk 47.

Arteta, Arteta: Mashabiki ndio Chachu ya Ushindi, Meridianbet

Ushindi huo unaifanya Arsenal kuweka rekodi yake ndani ya Europa League ikiwa imeshinda mechi zote tano na kujikusanyia pointi 15 nafasi ya kwanza kibindoni huku Rapid Wien ikiwa nafasi ya 3 na pointi 6 Kwenye kundi B.

Arteta amesema:”Mashabiki walitupa nguvu na kuwafanya wachezaji wapambane kwa juhudi kupata matokeo chanya hili ni jambo la faraja kwetu na mashabiki,”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Arteta, Arteta: Mashabiki ndio Chachu ya Ushindi, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

20 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa