Arteta: Timber Yuko Mbioni Kurejea

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ameweka wazi juu ya taarifa za urejeo wa beki wake Jurien Timber ambaye amekua na majeraha kwa muda mrefu sasa.

Kocha Arteta amesema kua beki Jurien Timber yuko mbioni kurejea ndani ya timu hiyo, Hii ni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu zaidi kwani beki huyo amekaa nje ya uwnaja kwa takribani msimu mzima.artetaBeki Jurien Timber alipata majeraha katika siku za mwanzo tu alipojiunga na timu hiyo jambo ambalo limemfanya kutoitumikia timu hiyo kwa katika mashindano mbalimbali msimu tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Ajax Amsterdam.

Beki huyo ameshaanza mazoezi baada ya kupona majeraha yake ya goti aliyoyapta na kumfanya kufanyiwa upasuaji, Lakini bado hajaanza kucheza mechi jambo ambalo linaonesha ni wazi atarejea uwnajani siku za hivi karibuni.

artetaKocha Mikel Arteta ameongeza kua beki Jurien Timber ana nafasi ya kuendelea kucheza msimu huu licha ya majeraha makubwa aliyoyapata, Beki huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi alidhaniwa hataweza kucheza tena msimu huu lakini mambo yamekua tofauti kwani atarejea ndani ya kikosi cha Arsenal hivi karibuni kabla ya msimu kumalizika.

 

Acha ujumbe